MsichanaTai App

Jiunge kwenye Vuguvugu la Tai.

Msichana Tai App ni interactive platform yenye  kuendeleza Vuguvugu la mabadiliko la “Msichana ni Tai” linalolenga kuwafikia wasichana milioni tano ndani na nje ya nchi ili waanze kujiamini kwamba wao ni Tai na sio Kuku.  Je wewe ni mmojawapo?  Kama jibu ni ndio, jiunge leo na pia mjulishe rafiki yako ili nae ajiunge.

Kwanini tunasema Msichana ni Tai?

Msichana ni Tai kwa sababu ana nguvu ya mabadiliko kwa kuyashinda yaliyopita na kubeba sifa za Tai ambazo zitamuongoza kufanikiwa katika maisha.

Msingi wa Vuguvugu

Msingi wa vuguvugu la mabadiliko ya kuwa Msichana ni Tai unatokana na imani ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (1944) kwamba wanawake wanapaswa kujiondoa katika hali ya udhaifu inayorithishwa na jamii kwa kuwaita kuku lakini ki uhalisia wanawake wana nguvu inayofananishwa na Tai.

Tai ni nani?

Tai ni mmoja kati ya aina ya ndege walio maarufu duniani. Ni viumbe wenye ishara ya nguvu , uhuru na dhamira ya kweli. Tai ni ndege aliye na sifa za kipekee hasa kutokana na ufundi wao wa kuwinda, uwezo wao wa kuona kwa macho. Anaona umbali mara saba zaidi ya jinsi anavyoona binadamu.

Kuhusu Vuguvugu

Shirika la Msichana Tai limeanzisha vuguvugu hili  la mabadiliko linalolenga kuwafikia wasichana Milioni Tano ndani na nje ya nchi ili waanze kujiamini na wanaamini kwamba wao ni Tai sio Kuku.

Mara nyingi wasichana wengi wamekuwa wakiamini kwamba wao ni viumbe dhaifu lakini ki ukweli Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliandika yafatayo:

“Wanawake meumbwa kwa mfano wa Mungu, lakini watu wamewafanya muamini kuwa nyie ni Kuku na nyie wenyewe imeamini hivyo; lakini nyie ni Tai, kunjua mbawa zenu na mruke, msihadaike na chakula cha kuku. Kwa uwezo wenu wenyewe  na  msaada wa marafiki zenu tokeni kwenye hali hii ya unyonge  ambayo mpo leo, ili muweze kufurahia uhuru na haki kwenye ulimwengu wa  amani”.

Hivyo basi vuguvugu hili linahamasisha hali za wasichana kuhoji mila na desturi kandamizi zinazowafikirisha kwamba wao ni kuku sio Tai Nyerere amesisitiza kunjueni mbawa zenu na mruke  nyinyi ni Tai na sio kuku.

Jiunge kwenye Vuguvugu

Loading…

Makala Zetu.

Our Stories

Tunawezesha Wasichana Kujiajiri
Simulizi Ya Malkia Nana
Msichana Ni Tai Sio Kuku